Washiriki 18 watetea mapendekezo yao kwenye Shindano la Pili la DLI “DREAMS”

Washiriki 18 watetea mapendekezo yao kwenye Shindano la Pili la DLI “DREAMS”

Washiriki 18 watetea mapendekezo yao kwenye Shindano la Pili la DLI “DREAMS”

Shindano la Ubunifu la Data for Local Impact (DLI) linawapongeza washiriki wote ishirini wa dirisha la pili la shindano kwa kufikia hatua ya kutetea hoja zao. Kati ya washiriki 20, washiriki 18 waliweza kushiriki vizuri katika tukio hilo wakitetea mapendekezo yao, wakichangia mawazo yao tofauti ya jinsi gani ya kuwalinda wasichana na wanawake vijana dhidi ya mazingira hatarishi ya kupata maambukizi ya VVU/Ukimwi.
Dirisha la pili la shindano lililenga kwenye vipaumbele vya serikali ya Tanzania katika Afya; na kuunga mkono mipango ya kimkakati ya PEPFAR inayoangazia masuala ya VVU/Ukimwi miongoni mwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana, ushirikiano huo unaojulikana kama DREAMS yaani Determined, Resilient, Empowered, AIDS Free, Mentored, and Safe). Ushirikiano wa DREAMS umewalenga wasichana na wanawake vijana walio katika mazingira hatarishi walio na wa miaka 10 – 24, ukiangazia zaidi kwa walio na umri wa miaka 15-24. Kundi hilo linaloangaliwa zaidi lipo katika hatari ya kupata maambukizi mara 2.5 zaidi kuliko washirika wao wa kiume. DREAMS imelenga katika kupunguza uwezekano huo kwa kundi hilo kwa kupunguza maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa wale walio na umri kati ya miaka 15-24 kwa asilimia 40 kupitia mchakato unaotegemea zaidi ushahidi maalum unaolenga zaidi makundi manne ya watu; Wanawake Vijana, Wanaowangalia, Washirika wao kimapenzi na wanajamii wao. Michakato hii imethibitika kuzuia miendeno hatarishi ya VVU, Usambaaji wa VVU na Ukatili wa Kijinsia.
Dirisha la Pili la Shindano la Ubunifu la DLI lilizinduliwa mnamo Mei tarehe 24, 2917 na kufungwa mnamo Julai tarehe 5, 2017. DLI ilipokea zaidi ya maombi 180. Baada kupitia mchakato thabiti na tathmini kutoka kwa jopo la majaji la wataalam watano nchini, maombi 20 yalichaguliwa na kufika hatua ya mwisho ya shindano – kutetea mapendekezo yao mbele ya jopo la majaji na hadhira katika ofisi za COSTECH jijini Dar es Salaam.
Akizungumza huku akiwa anahitimisha zoezi hilo, Bw. Agapiti Manday, Meneja Mradi wa DLI, aliwapongeza washiriki hao kwa kufikia hatua ya mwisho na kutetea vizuri mapendekezo yao yaliyosheheni mawazo tofauti yakibunifu. Bw. Manday aliwahasa washiriki hao kuongeza juhudi zaidi katika uboreshaji wa miradi yao kwa kujenga timu ambazo zitaendeleza mawazo yao na kuwa ufumbuzi yakinifu ambao unaweza leta mabadiliko chanya katika jamii zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

DLIIC : Welcome !

Authorize

Lost Password

Register