Tuma Maombi

Je upo tayari kwa shindano?

Pakua Kitabu cha Maelekezo kwa Muombaji, badilisha mawazo yako kuwa ufumbuzi, malizia maombi yako kupitia mtandao, na ushinde uweze kulitekeleza wazo lako!

Pakua Kitabu cha Maelekezo kwa Muombaji

( N.B. Maombi kwa sasa yamefungwa, endelea kutembelea tovuti kwa taarifa zaidi)

Mada Kuu

Shindano la dirisha hili limelenga katika Uwezeshaji wa Kiuchumi: Ajira na Ujengaji uwezo wa Ajira kwa Vijana. Mlengo huu unaunga mkono Lengo Endelevu la Maendeleo la 8, ambalo limelenga katika ukuaji wa uchumi ulioendelevu na wa kwapamoja, ajira kamilifu na zenye ufanisi na kazi nzuri kwa wote. Kwa maelezo zaidi juu ya mada kuu tafadhali fungua na kusoma Jarida la Muombaji yaani: Applicant Resource Book

Je Shindano la Ubunifu la DLI linatoa nini kwa washindi?

Washindi wa DLI Innovation Challenge watapata ruzuku ili kuwawezesha kuendeleza ufumbuzi uliopendekezwa kwa kipindi cha miezi 3-6. Mbali na kupata misaada ya kifedha, washindi watapewa mshauri ambaye atawasaidia kuendeleza mawazo yao ya ubunifu na kuwa kamili. Washindi pia watapata mafunzo na msaada wa usimamizi wa ruzuku kutoka kwa timu ya DLI.

Vigezo Vinavyohitajika – Je una vigezo?

Vigezo vya Tathmini

DLIIC : Welcome !

Authorize

Lost Password

Register