Dirisha la kwanza hadi lilipofunguliwa

Dirisha la kwanza hadi lilipofunguliwa

Dirisha la kwanza la DLI Innovation Challenge lililenga mashirika na watu binafsi   kutoka Tanzania nzima.

Uombaji wa ushiriki katika shindano hiulo ulianza kuanzia Oktoba 25 hadi Novemba 26 mwaka jana saa 6:00 usiku.

Dirisha hilo la kwanza liliwavutia waombaji wapatao   723 kutoka taasisi  190 ziulizosajiliwa na  533  kutoka kwa waombaji binafsi.

Hata hivyo ni taasisi  33  na watu binafsi  131 waliotimiza masharti ya uombaji.

Pia kati ya waombaji hao waliotimiza  masharti ya uombaji ni taasisi  11  na watu binafsi  118

Baada ya kukamilika mchakato huyo jopo kutoka kwa wabunifu na wataalamu wa afya nchini Tanzania  walikaa na kupitia masharti na vigezo yaliyoorodheshwa katika kitabu cha masharti kwa waombaji cha  DLIIC.

Baada ya kupitia kitabu hicho na kujiridhisha, jopo hilo la majaji lilikaa na kuteua orodha ya washindi wa mwisho ambapo taasisi nne na watu binafsi 22 waliofanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo na kupata nafasi ya kutetea mapendekezo yao kwa majaji jijini  Dar es Salaam.

Tukio hilo lilifanyika Desemba 3 mwaka jana katika Kitivo cha Takwimu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (Co-ICT)  na kuhudhuriwa na maofisa wa ngazi ya juu kutoka Mpango wa Changamoto za  Millennium  (MCC)  na Mpango wa Dharura  wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI  (PEPFAR).

Nafasi yetu  katika kuendesha  mchakato huu? Watu ambao ni wavumbuzi na wabunifu ambao tulikutana katika Dirisha la kwanza la walitupa nguvu  na kutuongezea msisimko katika utendaji wa kazi  zetu.

Wakati wa mchakato wa  kutafuta ushirikiano, timu yetu ya mradi ilikutana na waboreshaji  wa ndani 688  ambapo katika idadi hiyo walikuwapo  wanawake 124 katika vikao vya hana  kwa hana vilivyofanyika katika vyuo vikuu na vyuo vikuu vya uvumbuzi ili kuweza kuwaeleza malengo ya mpango huu wa  DLI.

Mbali na hao pia vilevile tuliweza kukutana na mamia kupitia  katika vyombo vya habari vya kijamii ili kujadiliana kuhusu  fursa hii na kujibu maswali yao kuhusu taasisi za nje na za ndani  zinazoomba  ruzuku  kutoka  DLIIC.

Kwa kupitia njia hii ya  mazungumzo yalituwezesha kuwasaidia wale waliokuwa  na maswali juu ya mpango huu, jinsi ya kujaza fomu ya maombi na kuwasilisha mawazo yao ambao matokeo yake yote unaweza kuyapata katika kurasa zetu za  Facebook  na  Twitter .

Tunatarajia utaendelea kushirikiana nasi ili kuweza kuongeza nguvu katika mpango wa dirisha la pili ambao unatarajia kuja hivi karibuni mapema Machi 2017.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

DLIIC : Welcome !

Authorize

Lost Password

Register