Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Majaji wamekuwa bize wakipitia maombi ya dirisha la pili na kuchagua mawazo yaliyo bora kwa ajili ya tukio la kuziwasirisha. Tunategemea kutangaza washindi ifikapo mwezi Septemba 2017. Tutembelee kupitia Twitter, Facebook, LinkedIn au Instagram na upate taarifa zaidi!

Ndiyo! Tutakuwa na dirisha lingine la shindano mwaka 2017. Mikakati tayari inakaribia kwa ajili ya dirisha letu la tatu la shindano. Tunaweza kukwambia kuwa mada zetu kuu zitalenga zaidi katika fursa za kiuchumi na utengenezaji wa ajira kwa vijana. Endelea kutembelea hapa kwa taarifa zaidi juu ya mada kuu na ratiba.

Wote! Aidha hii ni mara yako ya kwanza kusikia kuhusu shindano la Ubunifu la DLI au umeweza kufika mpaka hatua ya mwisho katika shindano la kwanza, tunakuhitaji uchangie mawazo yako ya kibunifu kwa ajili ya kukuza matumizi ya takwimu yaani data nchini Tanzania.

DLI Innovation Challenge hufadhiliwa na PEPFAR kupitia mpango wa MCC-PEPFAR DCLI na unalenga katika jitihada zinazohusiana na Afya na Ustawi (SDG 3), Usawa wa Jinsia (SDG 5), na Kazi Bora na Ukuaji wa Uchumi (SDG 8). Kabla ya kila dirisha la shindano, DTBi inatumia mchakato shirikishi na ushirikiano na wadau wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya serikali husika na taasisi nyingine zinazohusiana na eneo husika la shindano. Orodha ndefu ya mada kuu hupitiwa, kurekebishwa, kuendelezwa na kupimwa wataalam husika kabla ya kuchagua mada kuu za mwisho za shindano.

Yale yakibunifu! Tunayakubali mawazo mapya kwa ajili ya mchakato, mifumo, vifaa vya kimtandao. Pia tunakubali maombi yanayolenga kusaidia kukuza uvumbuzi/mradi. Angalia vigezo vya tathmini ili kuona kama wazo lako linaweza kuibuka mshindi. Mawazo yanapaswa kulandana na mada kuu za shindano aidha kukuza mahitaji ya takwimu zilizo bora au uwezo wa kutumia takwimu katika kuboresha maisha ya watanzania.

Ni raia wa Tanzania pekee walio na umri zaidi ya miaka 18 na zaidi ndiyo wenye vigezo vya kuomba. Taasisi ni lazima ziwe zimesajiliwa kisheria nchini Tanzania. Soma vigezo vyote katika kurasa yetu ya maombi kwa ajili ya taarifa zaidi.

Muombaji anapaswa kuchagua kuomba katika eneo moja tu – mtu binafsi au taasisi – kwa kila dirisha la shindano. Waombaji watakaoomba wakiwa kama watu binafsi na taasisi katika dirisha moja la shindano hawazingatiwa kwa ajili ya ruzuku.

Ni mtu wa kuwasiliana naye tu aliyopo kwenye maombi ndiyo anaehitaji  kuambatanisha kitamburisho na barua ya kumbukumbu na majina ya marefa. Hata hivyo, kama utachaguliwa kwa ajili ya ruzuku, wote waliopo kwenye timu watajumuishwa katika hatua ya kufanyiwa tathmini kabla ya utoaji ruzuku.

Watu binafsi na TImu ndogo ndogo wanaweza shinda mpaka Dola za kimarekani 25,000. Taasisi zilizosajiliwa zinawezashinda mpaka Dola za Kimarekani 100,000.

Fedha zina lengo la kusaidia kwa ufanisi kutafsiri wazo lako na suluhisho la ubunifu au bidhaa inayozungumzia moja kati ya mada kuu. Utahitaji kutoa ripoti ya maendeleo kuelekea kwenye lengo na jinsi unavyoweza kutumia fedha kwa Meneja wa Ruzuku wa DTBi na/au mshauri wako.

Mbali na kupokea pesa, washindi wataunganishwa na washauri katika maeneo yao. Mshauri huyu atasaidia katika kuendeleza mawazo yao ya ubunifu mpaka kuwa bidhaa iliyokamilika.

Utakuwa unasaidia kuungamkono hitaji la watanzania na kuboresha maisha wakati pia ukijenga ujuzi wa uundaji, utekelezaji, usimamizi, ufuatiliaji na ufanyaji wa tathmini. Ukiwa kama mshiriki katika Shindano la ubinifu la DLI, utakuwa pia na fursa ya kukutana na kushirikiana na wabunifu wengine wa kitanzania, waendelezaji, wataalam katika takwimu, na watoa ufumbuzi. Kwa kujiunga na Shindano la Ubunifu la DLI kutakuwezesha wewe baadae kupata fursa za kuboresha matumizi ya takwimu na kufanya mabadiliko makubwa katika maisha ya watu.

JE UNA WAZO LA KIBUNIFU?

DLIIC : Welcome !

Authorize

Lost Password

Register