Uwezeshaji wa wagunduzi nchini Tanzania

Uwezeshaji wa wagunduzi nchini Tanzania

Shindano la Ugunduzi kwa kutumia Data lijulikanalo kama Data for Local Impact Innovation Challenge (DLIIC) hivi karibuni limechagua washindi wagunduzi 12 waliopata tuzo zenye lengo la kutatua changamoto mbali mbali katika sekta ya afya Tanzania. DLIIC inafadhiliwa na serikali ya Marekani chini ya Mpango wa Rais wa Dharura unaosimamia masuala ya upungufu wa kinga mwilini yaani President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) ikilenga kusaidia jamii ya Tanzania katika utumiaji wa Data na kuboresha sekta ya afya huku Dar es Salaam Business Incubator (DTBi) ikishirikiana na shirika la Palladium katika utekelezaji wa mradi huo wa DLIIC.

Washindi 12 wa Dirisha la Kwanza la Shindano la DLIIC wakionyesha vyeti vyao baada ya kuibuka washindi wa Shindano hilo mnamo Machi 2017.
Washindi 12 wa Dirisha la Kwanza la Shindano la DLIIC wakionyesha vyeti vyao baada ya kuibuka washindi wa Shindano hilo mnamo Machi 2017.

Katika Dunia nzima, maamuzi muhimu katika masuala ya afya, maendeleo, mgawanyo wa rasilimali mara nyingi utokana na taarifa zisikamili, zisizopatikana kwa urahisi na zisizosahihi. Changamoto katika uzalishaji wa data, ubora, upatikanaji wake, na utumiaji unazuia ufanyaji maamuzi sahihi. Hatahivyo, hali hiyo inabadilika. Mifumo ya upatikanaji wa data imejitokeza, na teknolojia mpya imeweza kuboresha upatikanaji na utumiaji wa data. Upatikanaji wa data umekuwa ni rahisi kupitia mpango wa serikali wa kuwezesha upatikanaji wa data-zilizowazi na upeanaji wa data kupitia vyombo mbali mbali binafsi.

Baada ya kufikia mafanikio ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia, Serikali ya Tanzania imejikita katika kufikia mafanikio ya Malengo Endelevu ya Maendeleo. Ili kufikia malengo haya, Serikali imejidhatiti katika kutanua na kuboresha matumizi ya data na teknolojia na kuimarisha ubora wa huduma zake za afya.

Katika miaka michache iliyopita, serikali ya Tanzania imezidi kuwezesha upatikanaji wa data za afya kwa umma ili kutoa uwazi mkubwa na kuboresha miradi mbali mbali ya afya. Hatahivyo, utoaji wa data kwa umma hauthibitishi matumizi madhubuti ya data. Bado kuna fursa na changamoto za kuhusisha na kuwajengea uwezo jamii na wagunduzi wa ndani ili kutumia vizuri taarifa katika kufikia vipaumbele vya taifa katika sekta ya afya.

Mmoja kati ya washindi Bw. Bukhari Kibonajoro akionyesha cheti chake.
Mmoja kati ya washindi Bw. Bukhari Kibonajoro akionyesha cheti chake.

Je DLIIC ni nini?
“Data for Local Impact Innovation Challenge imelenga kuwaleta pamoja, kuwasaidia na kuwaunganisha wagunduzi wakitanzania, waendelezaji na watoa tatuzi kwa pamoja lakini kuwaunganisha na fursa mbali mbali ili kufanya mabadiliko chanya katika maisha ya watu,” alisema Agapiti Manday, Meneja Mradi wa DLIIC.

Shindano la DLIIC linafadhiliwa na serikali ya Marekani kupitia President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) na moja kati ya miradi inafadhiliwa na PEPFAR ya Data Collaboratives for Local Impact (DCLI). Kupitia Nyanja mbali mbali za uwekezaji, lengo la mpango wa DCLI ni kuwezesha na kuonyesha matumizi madhubuti ya data katika kukabiliana na HIV/AIDS, uboreshaji wa Afya, kukuza usawa wa kijinsia na kukuza uchumi. Hususani, imelenga taifa na serikali za mitaa, na wananchi katika kuboresha sera na mipango; kupeleka mbele gunduzi mbali mbali; na kukuza uwazi, uwajibikaji na ufanisi.

Mradi wa Dola za Kimarekani Milioni 21.8 wa DCLI ulizinduliwa mwezi Aprili 2015 ukipewa fedha toka PEPFAR na kusimamiwa na Millennium Challenge Corporation. Mradi huo unalandana na jitihada kubwa za serikali ya Marekani za, kusaidia nchi za nje, Digital Gap Act of 2017, na Mashirikiano ya kidunia kwa ajili ya Maendeleo Endelevu ya Data. Ambayo yamelenga kukuza ushirikishwaji wa data katika kufikia Malengo Endelevu ya Maendeleo.

In collaboration with the Dar es Salaam Teknohama Business Incubator (DTBi), Palladium is helping to implement the DLI Innovation Challenge in Tanzania. The DTBi-Palladium team is awarding grants to Tanzanians (both individuals and organisations) who have creative ideas about how to use or combine data in new ways to gain insights or empower people through access to life-changing information.

Kwa kushirikiana na Dar es Salaam Teknohama Business Incubator (DTBi), shirika la Palladium linasaidia katika utekelezaji wa mradi wa DLI Innovation Challenge nchini Tanzania. Timu ya DTBi- Palladium imewazawadia msaada watanzania (Watu Binafsi na Taasisi) ambao wanamawazo ya kibunifu juu ya jinsi gani ya kutumia au kuunganisha data kwa njia za kisasa ili kupata tatuzi au kuwawezesha watu kupitia upatikanaji wa taarifa yakinifu zenye uwezo wa kubadirisha maisha ya watu.
Kusherehekea mawazo yakibunifu.

Dirisha la kwanza la Shindano la DLI lilifanyika kwenye miezi ya Oktoba na Novemba mwaka 2016, likiwa limelenga zaidi Nyanja kuu Tatu:
1. Upatikanaji wa taarifa sahihi za huduma ya afya
2. Uwezeshaji wa Wananchi katika Upunguzaji wa Utoro kwa Wasichana mashuleni
3. Upatikanaji wa Mrejesho toka kwa Jamii Juu ya Ubora wa Huduma ya Afya.

Maombi yote yalitakiwa aidha kuzalisha au kutumia data zilizopo wazi, kuwa tayari ndani ya miezi mitatu, na kulenga masuala yanayowahusu vijana, wanawake vijana, jamii ya ngazi ya chini. Tatuzi hizo pia zilitakiwa kulenga japo moja kati ya wilaya 83 ambazo zimetengwa kuwa kama maeneo yenye kipaumbele kikubwa chini ya Mpango wa Kiundeshaji wa Nchi ya Tanzania wa PEPFAR wa mwaka 2017 yaani PEPFAR 2017 Tanzanian Country Operational Plan, ambao ulianzishwa kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania.

Kutoka maombi 129, wagunduzi 12 walizawadiwa fedha kama msaada ili kutekeleza miradi iliyolenga kutumia data mbali mbali katika kutatua changamoto katika sekta ya afya. Wajasiriamali hawa watapatiwa tuzo hizo zitakazoanzia kutoka Dola za Kimarekani 7000 mpaka 25000, ikiwa ni pamoja na msaada wa kitaalam kutoka kwa wataalam mbali mbali wa jinsi gani ya kuitekeleza miradi yao tofauti ya kijamii. Washindi hao walianza mafunzo yao mwezi Machi 2017, na kuanza utekelezaji wa miradi yao kati ya miezi ijayo mitatu au sita. Uzoefu huu utaboresha ujuzi wao wa jinsi ya kuendesha miradi kwa vitendo, Ujuzi wa kibiashara, uwezo wa kutumia data kisayansi. Muhimu zaidi, wagunduzi hawa wataleta tofauti kubwa katika maisha ya jamii zinazowazunguka na maisha ya watanzania kwa ujumla.

Kama tulivyojifunza kupitia shindano la ugunduzi la DLI, thamani ya data inapatikana pale inapotumika katika kutambulisha maamuzi ya kisera, kuwaunganisha watu na huduma za afya, kutambua chanzo cha utoro mashuleni, kuwawezesha wananchi kupaza sauti juu ya mahitaji yao katika huduma za afya, na njia nyinginezo nyingi ambazo matumizi madhubuti ya data yanaweza kuleta Mabadiliko Chanya na mabadiliko katika Jamii.
Kupitia ushirikiano wa karibu na serikali ya Tanzania, shindano la DLI la ugunduzi limetambua na kuwajengea uwezo wagunduzi wakitanzania katika kubadilisha data kuwa tatuzi za kiafya na kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

DLIIC : Welcome !

Authorize

Lost Password

Register